Julia Montes Swahili Biography







Mara Hautea Schnittka amezaliwa March 19, 1995 ni maarufu kwa jina la Julia Montes, ni muigizaji, mwanamitindo, mtangazaji na muandaaji wa filamu kutoka nchini Philippine. Amezaliwa nchini Philippine na mamayake ambaye ni kiziwi anaitwa Gemma Hautea ambaye ni Mfilipino na baba yake Martin Schnittka. Schnittka ambaye ni Mjerumani. Baba yake aliondoka kipindi Julia akiwa mdogo sana na kuiacha familia yake na alilelewa na mama yake ambaye ni kiziwi kwa msaada wa bibi yake Flory Hautea ambaye hakuwa na uwezo sana. Mbali na Julia pia ana wadogo zake wawili ambao ni Patrick and Paolo walie share mama ila kila mmoja ana baba yake.

Katika maisha yake aliamini kwamba elimu ndio njia pekee ya yeye kupata maisha bora, katika umri mdogo alikuwa akujishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni njia ya kupata chochote kwa ajili ya familia yake. Akiwa na miaka mitano alianza kujitokeza kutafuta nafasi katika makampuni yaliyo kuwa yakitafuta watoto kwaajili ya matangazo. Akiwa na miaka mitano alifanikiwa kupata nafasi ya kuwa mwanamitindo mtoto na kwa malipo aliyokuwa akiyapata yalichangia kubadili maisha yake na ya familia yake

Mwaka 2001 akapata nafasi ya kuigiza katika tamthilia ya It Might be you iliyo kuwa chini ya GMA na huo ulikuwa mwanzo wa maisha yake katika tasnia ya uigizaji. Mwaka 2004 akapata nafasi ya kuigiza kama muigizaji mualikwa katika tamthilia ya Hirram na baadaye mwaka huo huo akaigiza tena kwenye MMK kama muigizaji mualikwa ambazo zilimpa nafasi ya kupata kutangaza kipindi cha watoto Goin' Bulilit. Aliendelea na utangazaji wa kipindi cha watoto wakiwa na rafiki yake kipenzi Kathryn Bernardo na pia wakiendelea kuigiza katika nafasi tofauti tofauti. Mwaka 2010 ABS-CBN wakaingia katika mkakati wa kuirudia tamthilia ya Mara Clara na alichaguliwa kama Muigizaji mualikwa na muigizaji mkuu msaidizi katika tamthilia ya Mara Clara. Ili kuondoa mkanganyiko wa jina lake halisi na nafasi aliyo kuwa akiigiza aliamua kubadili jina lake kutoka Mara Montes na kuwa Julia Montes hivyo mpaka leo ndilo limekuwa jina lake maarufu, jina lake la kisanaa, na jina lake la pili. Mafanikio yake kwenye Mara Clara yalikuwa makubwa sana kutokana na kuotendea haki nafasi aliyo pangiwa kuiigiza. Mafanikio yao katika Mara Clara iliwapelekea waandaaji wa tamthilia wa ABS-CBN kuandaa filamu nyingine mwaka 2011 ya Way Back Home iliyo wakutanisha tena Julia, Kathryn na Enrique Gill. Mwaka 2011 tena ABS-CBN wakawaunganisha tena katika tamthilia ya vichekesho ya Growing Up ikiwa ni kwa mara ya kwanza Daniel Padilla akijiunga na Kathryn na Julia.

Mwaka 2012 akafanya vizuri sana na tamthilia ya My Eternal (Walang Hanggan) aliyo igiza na Coco Martin, tamthilia hii ilipelekea mashabiki kutaka Coco na Julia kuwa wapenzi. Mafanikio ya My Eternal ikapelekea kuwa love team inayopendwa zaidi ya CocoJulia na mwaka mmoja baadaye wakarudi na filamu ya A Moment In Time iliyo wapa tuzo ya heshima ya Prince and Princess of Philippines Drama kwa Coco Martin na Julia Montes. Mwaka 2013 akaigiza If Only (Muling Buksan Ang Puso) iliyo endelea kumpa heshima na kujizolea washabiki lukuki. Baada ya malalamiko ya wengi kupenda kuwaona tena kwenye tamthilia pamoja Coco Martin na Julia Montes mwaka 2014 wakaigiza pamoja kwenye tamthilia ya No Great Love (Ikaw Lamang).

Kwa kudhihiriaha yeye ni bora mwaka 2015 akapewa nafasi ngumu sana ya kuigiza nafasi mbili kwa wakati mmoja Doble Kara, taarifa zisizo rasmi zinasema Doble Kara wasanii wengi waliogopa kuigiza kutokana na hadithi kuwa ngumu. Julia anasifika kwa kutotegemea love team katika uigizaji wake tofauti ilivyo kwa KathNiel (Kathryn Bernardo na Daniel Padilla), alifanya vizuri alipo kuwa na Coco Martin, akafanya vizuri na Enrique Gill, akafanya vizuri na Gerald Anderson na wengine wengi. Mwaka 2018 akapewa nafasi ya kuwa muigizaji mkuu kwenye tamthilia ya Asintado akiwa na Paul Avelino kama muhusika mkuu msaidizi.

Maisha yake binafsi mwaka 2015 alimaliza kozi ya mapishi katika chuo cha Center for Culinary Arts. Mbali na mafanikio katika uigizaji na uana mintindo anakadiriwa na kuwa na utajiri wa kufikia $180, anamiliki nyumba 3, migahawa, saloon na duka la nguo. Rafiki yake mkubwa ni Kathryn Bernardo na walimekua na kucheza pamoja licha ya tofauti za kifedha walizokuwa nazo, katika maisha yao ya utotoni Kathryn alisha wahi kamatwa akiiba sukari na baadhi ya vitu kumpelekea Julia walio kuwa wakisoma shule mbili tofauti zilizo kuwa zikipakana. Kathryn amekuwa mmoja ya watu walio msaidia Julia kuingia katika tasnia ya uigizaji. Julia ni muumini wa imani ya kikristo (Katoliki), amekuwa akiamini katika maisha yake kwamba kila jambo hutokea kwa makusudi yake na makosa hupaswa kusamehewa  December  mwaka 2016, mashabiki zake wakishirikiana na binamu yake Michelle Lloyd walifanikiwa kumkutanisha na baba yake mzazi Martin Schnittka ambaye hakuwahi kumfahamu toka alipo zaliwa.

Julia hana mtoto na mhusiano yake yamekuwa ya siri japo inaaminika ya kwamba yupo kwenye mahusiano na Coco Martin.

Popular posts from this blog

Ina, Kapatid, Anak "Her Mother's Daughter"

Walang Hanggan "My Eternal"

Endless Love Philippine Drama